Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yafanya dua maalum kwa ajili ya Yusuf Manji

Hersiii 68x614.jpeg Yanga yafanya dua maalum kwa ajili ya Yusuf Manji

Mon, 8 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Yanga kwa kushirikiana na wazee wa klabu hiyo, wamefanya dua maalum ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti na Mfadhili wa Klabu yetu, Marehemu Yusuf Manji aliyefariki dunia, Juni 30, 2024.

Rais wa Yanga, Eng Hersi Said, amewaongoza wazee wa Yanga kwenye dua hiyo maalumu iliyofanyika Makao Makuu ya Klabu ya Yanga, Jangwani jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika dua hiyo, Eng Hersi ameanza kwa kuwashukuru wote waliohudhuria huku pia akibainisha kwamba Manji aliipambania Yanga katika kipindi chake na klabu kupata mafanikio.

“Nawashukuru sana wazee wetu na wadau ambao wamejitokeza kwenye dua hii maalumu kwa ajili ya kumuombea aliyekuwa Mdhamini, Mfadhili na Mwenyekiti wetu, Yusufu Manji kama sehemu ya kuungana na familia yake.

“Sisi sote tumefurahishwa sana na jitihada za Yusuf Manji ambazo alifanya kwa klabu hii. Manji alifanya mambo makubwa sana kuhakikisha kuwa klabu yetu hii inapata mafanikio. Katika utawala wake amefanya mambo mengi mazuri mno. Katika wakati wake tulipata mafanikio makubwa.

“Dua hii ni kuthibitisha kuwa tuna enzi yake yote mazuri aliyofanya kwa klabu yetu. Mafanikio ambayo Yanga tumepata kupitia kwa Manji yataendelea kubaki kwenye historia na mioyo ya kila mdau na mpenzi wa soka letu,” alisema Eng Hersi.

Manji aliyefariki akiwa nchini Marekani na kuzikwa huko, alikuwa Mwenyekiti wa Yanga kuanzia 2012 hadi 2017.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live