Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaendeleza ubabe kwa Singida, Nzengeli wa moto

Yanga 2 0 Singida Yanga yaendeleza ubabe kwa Singida, Nzengeli wa moto

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga SC wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Singida Big Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Nyota wa mchezo wa leo ni kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Maxi Mpia Nzengeli aliyefunga mabao yote mawili, dakika ya 30 na 39.

Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 18 katika mchezo wa saba na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tatu zaidi ya Simba SC ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi.

Kwa upande wao, Singida Big Stars wanabaki na pointi zao nane na wanashuka kwa nafasi moja hadi ya 10 baada ya wao pia kucheza mechi saba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: