Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaendeleza ubabe kwa Mkapa, Yaongeza dozi

Full Time Pic Data Yanga yaendeleza ubabe kwa Mkapa, Yaongeza dozi

Tue, 2 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Dar es Salaam. DAKIKA 90, zimetamatika katika Uwanja wa Benjamini Mkapa kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-1, dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Kipindi cha kwanza kilianza kwa kasi na nguvu kubwa baada ya timu zote mbili kulazimisha sare ya 1-1 huku Ruvu Shooting wakienda mapumziko baada ya nahodha wao Santos Mazengo kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 24.

Bao la Ruvu Shooting limefungwa na Shaban Msala dakika ya 10, baada beki wa Yanga Dickson Job kuugusa Mpira na kumpoteza golikipa Djigui Diarra.

Kocha wa Ruvu Boniface Mkwasa alilazimika kufanya mabadiliko ya kumtoa Marcel Kaheza na kumuingiza beki Ally Mtoni ili kuongeza nguvu kwenye eneo la ulinzi.

Mshambuliaji wa Yanga Yacouba Sogne alipata majeraha na kushindwa kuendelea na mchezo huku nafasi yake ikichukuliwa na Saido Ntibanzonkiza.

Yanga iliendelea kulishambulia lango la Ruvu Shooting ambapo dakika ya 32, Feisal Salum 'Fei Toto' aliipatia Yanga bao la kusawazisha baada ya kupiga shuti kali nje ya 18, lililomshinda golikipa Mohamed Makaka.

Related Ruvu Shooting yaitoa kijasho Yanga 45 za kwanza Ruvu yaapa kuanza kuifunga Yanga leo Yanga mipasi mingi, bao! Aucho, Bangala levo za mbaliYanga iliendelea kushambulia lango la Ruvu Shooting ila mpaka dakika 45, za kipindi cha kwanza zilimalizika timu hizo zikifungana bao 1-1.

Kipindi cha pili Yanga ilianza kwa kasi ambapo dakika ya 46, ilipata penalti baada ya mlinzi wa Ruvu Shooting Ally Mtoni 'Sonso' kuunawa mpira uliopigwa na Feisal Salum 'Fei Toto' kwenye eneo la hatari.

Beki Djuma Shaban aliipatia Yanga bao la pili baada ya kupiga penalti ya kiufundi iliyomshinda golikipa wa Ruvu Shooting Mohamed Makaka.

Dakika 65, Yanga ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Kibwana Shomari na Jesus Moloko, huku nafasi zao zikichukuliwa na David Bryson pamoja na Farid Mussa.

Mabadiliko hayo yalileta tija kwa Yanga baada ya dakika ya 75, kiungo Mukoko Tonombe kuipatia Yanga bao la tatu akiunganisha krosi safi ya Farid Mussa.

Dakika ya 80, Yanga iliendelea kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Mukoko Tonombe na Feisal Salum na nafasi zao zikichukuliwa na Yusuf Athuman pamoja na Zawadi Mauya.

Feisal Salum 'Fei Toto' anakuwa mchezaji wa Yanga anayeongoza kuifunga mara nyingi Ruvu Shooting ambapo bao lake la leo linakuwa ni la nne tangu msimu wa 2017/18.

Katika misimu minne timu hizi zilipokutana Yanga inaongoza kuifunga Ruvu Shooting mabao 16, na kuifanya kuendeleza ubabe kwani katika michezo 11, iliyopita Ruvu imeibuka na ushindi mara moja ambapo ilikuwa ni Agosti 28, 2019.

Kwa matokeo haya Yanga inaendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara ikifikisha pointi 15, baada ya kushinda michezo yote mitano huku Ruvu Shooting ikipoteza mchezo wa tatu msimu huu baada ya kufungwa bao 1-0, na Polisi Tanzania pamoja na Dodoma Jiji bao 1-0 kwenye mechi ya kwanza ya ufunguzi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz