Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaendeleza ubabe kwa Azam FC, Aziz Ki wa moto

Aziz Ki Vs Azam FC Leo Yanga yaendeleza ubabe kwa Azam FC, Aziz Ki wa moto

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bra Timu ya Yanga imeendeleza ubabe mbele ya matajiri wa Jiji Azam FC baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania ulikuwa na ushindani wa hali ya juu huku kila Timu ikihitaji alama tatu ili kujikita katika uongozi wa msimamo wa Ligi.

Yanga ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Kiungo wao stephen Aziz Ki mapema katika dakika ya 9.

Azam FC walisawazisha kupita kwa Silla dakika ya 19 na kuafnya matokeo kuwa 1-1 dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika.

Kipindi cha pili Azam walirudi kwa kasi na kujipatia bao dakika ya 62 likiwekwa wavuni na Prinvce Dube kwa mkwaju wa Penati.

Stephen Aziz KI kwa mara nyingine akapachika mabao mawili dakika za 69 na 72 na kuwarudisha Wananchi mchezoni.

Mpaka dakika 90 zinakamilika Yanga wakachukua alama zote tatu na kukwea mpaka kileleni mwa msimamo wa Ligi wakiwa na alama zao 15 sawa sawa na Simba huku wakitofautiana idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa lakini Simba wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: