Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaendeleza rekodi Ligi Kuu, yaichapa Ruvu Shooting

Mwamnyeto Yanga Mk.jfif Yanga yaendeleza rekodi Ligi Kuu, yaichapa Ruvu Shooting

Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imeendelea kutoa matokeo mazuri kwenye ligi ya NBC baada ya jana kuibuka mshindi wa 2-1 na kujinyakulia pointi tatu dhidi ya Ruvu Shooting, mechi ambayo imepigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Ruvu Shooting walicheza kandanda murua kwenye mchezo huo katika kipindi cha kwanza licha ya kutengeneza nafasi kadhaa na kushindwa kuzitumia vizuri na kufanya matokeo kuwa 0-0 kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili Yanga iliingia ikiwa imeimarika kwani walibadika kwa kiasi kikubwa na kufanikiwa kupata bao la kwanza kupitia kwa Feisal Salum ambaye alipata bao akipokea krosi nzuri kutoka kwa Joyce Lomalisa.

Bao la pili la Yanga Sc liliwekwa kimyani na nahodha wao Bakari Mwamnyeto ambaye ni goli lake la pili kwa msimu huu 2022/2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live