NDOTO za Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu zimezidi kufi fi a kufuatia matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha jana. Hiyo ni mechi ya pili mfululizo kwa Yanga kushindwa kupata ushindi katika mechi mbili walizocheza ugenini hivi karibuni, baada ya kipigo cha bao 2-1 dhidi ya Coastal Union katikati ya wiki iliyopita.
Pia sare ya jana inakuwa ya nne kwa Yanga tangu kuanza kwa mzunguko wa pili msimu huu, ilianza kupata sare dhidi ya Tanzania Prisons, Mbeya City, na Kagera Sugar.
Sare ya jana imezidi kutoa nafasi kwa mabingwa watetezi Simba kukaa kileleni endapo itashinda mechi zake nne za viporo ambazo zitaiwezesha kufikisha pointi 57. Katika mechi ya jana, kiungo mshambuliaji, Fiston Abdulirazak aliifungia Yanga bao la kuongoza akiunganisha kwa kisigino pasi ya Tuisila Kisinda, lakini mchezaji wa zamani wa Yanga, Pius Buswita akaisawazishia Polisi dakika ya 89 na kufanya matokeo kuwa 1-1 dakika 90.
Yanga iliutawala mchezo kwenye eneo la kiungo hasa kupitia kwa mkongwe Haruna Niyonzima ambaye jana alianza kikosi cha kwanza pamoja na Feisal Salum na Tonombe Mukoko. Kipindi cha pili Polisi walionekana kuchachamaa kwa kufanya mashambulizi mengi kwenye lango la Yanga, lakini kipa Metacha Mnata na walinzi wake, Said Juma na Bakar Mwamnyeto waliyadhibiti.
Dakika ya 87, Polisi walilazimika kucheza pungufu baada ya beki wake mkongwe Kelvin Yondan kumchezea rafu Fiston na kuoneshwa kadi ya pili ya njano.
Katika mechi nyingine za ligi zilizochezwa jana, Mtibwa Sugar wakiwa nyumbani uwanja wa Jamhuri walipokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Gwambina FC, wakati Coastal Union wakiwa nyumbani uwanja wa Mkwakwani wakalazimishwa suluhu na KM