Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaendelea kujifua Sauzi

Yanga Sauziiims Yanga yaendelea kujifua Sauzi

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jana asubuhi, kikosi cha timu ya Young Africans kilifanya mazoezi kwa makundi mawili.

Mazoezi hayo yalifanyika siku moja baada ya juzi kucheza mechi ya Mpumalanga Cup dhidi ya FC Augsburg inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani maarufu Bundesliga.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Young Africans, Ally Kamwe, amezungumzia maendeleo ya kikosi hicho kilichopo Afrika Kusini na ratiba ya mazoezi ilivyokuwa.

“Kikosi kimefanya mazoezi asubuhi leo kwa makundi mawili. Kundi la kwanza ambalo wachezaji hawakucheza jana na waliocheza dakika chache.

“Kundi la pili limehusisha wachezaji waliocheza mchezo wa jana kwa dakika nyingi,” alisema Kamwe.

Kikosi hicho bado kipo Afrika Kusini kwa ajili ya pre-season tour kikiwa na mwaliko maalum kutoka timu za Afrika Kusini ambazo ni TS Galaxy na Kaizer Chiefs.

Katika mwaliko huo, tayari Yanga wamecheza mechi moja ya Mpumalanga Cup dhidi ya Augsburg kisha Julai 24 watacheza dhidi ya TS Galaxy mechi ya pili ya michuano hiyo.

Baada ya hapo timu itaondoka Mji wa Mpumalanga na kuelekea Johannesburg kucheza mechi ya Toyota Cup dhidi ya Kaizer Chiefs Julai 28, kisha kikosi kitarajea Dar es Salaam Julai 30 kuendelea na maandalizi ya Wiki ya Mwananchi itakayofanyika Agosti 4 Uwanja wa Benjamin Mkapa.

View this post on Instagram

A post shared by Young Africans Sports Club (@yangasc)



View this post on Instagram

A post shared by Young Africans Sports Club (@yangasc)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live