Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaenda Zanzibar kwa Kombe la Mapinduzi

91503193ce3afa37851378383796fe5f Yanga yaenda Zanzibar kwa Kombe la Mapinduzi

Sat, 9 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KIKOSI cha Yanga leo kinakwenda Visiwani Zanzibar tayari kwa Mashindano ya Kombe la Mapinduzi 2021 yatakayoanza kutimua vumbi kuanzia kesho Jumatano.

Yanga kwenye mashindano hayo, wamepangwa katika Kundi A pamoja na timu za Jamhuri ya Pemba na Namungo FC ya mkoani Lindi.

Akizungumza Dar es Salaam jana kocha wa Yanga, Cedric Kaze alisema kikosi chake hakijawajumuisha wachezaji waliopo katika timu ya taifa, Taifa Stars, ambao wameanza maandalizi kwa ajili ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa nyumbani, Chan, itakayofanyika Cameroon.

“Wachezaji wengine waliosalia wote tutasafiri nao kwenda Zanzibar na lengo ni kufanya vizuri katika mashindano hayo ili kuendelea kuwafurahisha mashabiki wetu, “alisema Kaze.

Kaze alisema licha ya kupanga kuchukua kila Kombe watakaloshiriki, lakini katika michuano hiyo wamepanga kuwapa nafasi zaidi wachezaji wao, ambao huwa hawapati nafasi ya kuanza katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika michuano hiyo kikosi cha Yanga kitaanza kucheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Jamhuri FC utakaofanyika Januari 7 kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanziabar na wanatarajia mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wao.

Mashindano ya hayo safari hii yatashirikisha timu tisa kutoka Tanzania Bara na visiwani humo ambazo ni Yanga, Namungo FC na Jamhuri FC Kundi A, Kundi B linaundwa na Simba, Mtibwa Sugar na Chipukizi FC huku Kundi C lina Azam, Mlandege na Malindi.

Chanzo: habarileo.co.tz