Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaeleza hali ya Aucho, Pacome, Kibwana, Mauya na Yao

F Aucho Yanga yaeleza hali ya Aucho, Pacome, Kibwana, Mauya na Yao

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Young Africans SC, Ally Kamwe ametoa ripoti ya hali za afya za majeruhi wa Klabu hiyo ambao ni Kibwana Shomari, Khalid Aucho, Yao Attohoula, Zawadi Mauya na Pacome Zouzoua.

Pacome na Yao, waliumia katika mchezo dhidi ya Azam, Kibwana majeraha alipata walipocheza dhidi ya Geita Gold, wakati Aucho akiumia walipovaana na Al Ahly, mechi ya mwisho ya Kundi D kunako Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Mauya akiwa ni majeruhi wa muda mrefu kidogo.

Kuhusu hali zao kwa sasa, Kamwe amesema: “Kibwana Shomari ataanza mazoezi mepesi hivi karibuni. Khalid Aucho anaendelea na sehemu ya pili ya mazoezi. Zawadi Mauya hali yake imeimarika.

“Yao Attouhoula alichanika nyama za paja na hali yake ni 50/50 kucheza mchezo wa Mamaelodi. Pacome aliumia goti, bado tunasubiri majibu kutoka kambi ya timu ya taifa.”

Kutokana na maendeleo mazuri waliyonayo nyota hao, kuna asilimia kubwa ya kuwepo fiti kukabiliana na Mamelodi Sundowns katika mchezo wa robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Machi 30, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live