Msafara wa wachezaji 25, benchi la ufundi 11, viongozi na mashabiki 15 wa Yanga SC wanatarajia kusafiri siku ya Jumamosi, Oktoba 15, 2022 kuelekea Sudan, kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal.
Yanga itaondoka nchini kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar Es Salaam, majira ya saa 10:00 alfajiri kwa Shirika la ndege ya Ethiopia na watatua Sudan, saa 6:40 mchana za saa Tanzania (Sudan itakuwa saa 11:40 asubuhi).
Baada ya mapumziko, kikosi cha Yanga kitafanya mazoezi saa 2:00 usiku kwa saa za Sudan, sawa na saa 3:00 usiku kwa saa za Tanzania, kwenye uwanja wa Al Hilal utakaotumika siku ya mchezo.
Baada ya mchezo, timu itarejea Tanzania Oktoba 17, 2022 kwa Shirika la Ndege la Ethiopia, majira ya saa 9:30 usiku kwa saa za Sudan na kutua nchini saa 6:45 mchana kwa saa za Tanzania.
Yanga wanataka kusafiri kama walivyosafiri watani zao Simba walipoenda Angola ambapo waliondoka siku Moja kabla ya Mchezo huku wakifanyiwa vipimo vya Corona Tanzania ili kukwepa figisu za kufanyiwa vipimo upya wakiwa Nchini humo.
Kikawaida Vipimo vya Corona hudumu Kwa masaa 72 (siku tatu) Kwa maana hiyo Yanga watafanyiwa vipimo vya Corona wakiwa Tanzania ambavyo vitadumu Kwa masaa 72 ikiwa ni mda sawa na watakaofika na kuondoka Nchini Sudan.