Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yabisha hodi Moro, Djuma Shabani ndani

YANGA KIKOSI Yanga ipo safarini kuifata Mtibwa Mkoani Morogoro

Mon, 21 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga kimeondoka mchana wa leo Februari 21, 2022 kuelekea Manungu Turiani Mkoani Morogoro kuwafuata walima miwa wa mkoa huo klabu ya Mtibwa Sukari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania utakaochezwa Jumatano ya Februari 23,2022.

Kuelekea kwenye mchezo huo, Afisa Msemaji wa Yanga, Haji Sunday Manara amethibitisha Yanga watawakosa wachezaji wake nyota watatu, Abdallah Shaibu Ninja, Bryson David na Jesus Ducapel Moloko kutokana na nyota hao wanasumbuliwa na majeraha.

Taarifa nzuri kwa wapenzi wa Yanga ni kurejea kwa mlinzi wake wa kulia, Djuma Shabani ambaye amemaliza kutumikia adhabu ya michezo mitatu kutoka na kumpiga usoni Yahya Mbegu wa klabu ya Polisi Tanzania mapema mwezi huu.

Mbali na Djuma Shabani, Manara amesema wachezaji Kibwana Shomari, Yassin Mustapha na Salum Aboubakar ‘Sure boy’ walishaanza mazoezi ya pamoja na timu hivyo wapo fiti ni suala la Kocha wa kikosi hicho, Mohammed Nasreddine Nabi kuwatumia ama laa.

Yanga SSC watacheza na Mtibwa Sukari Jumatano Februari 23, 2022 saa 10:00 jioni kwenye dimba la Manungu Turiani mji kasoro Bahari, Morogoro wakiwa vinara vinara wa Ligi Kuu NBC Tanzania wakiwa na alama 36 wakati Mtibwa wa 15 wakiwa na alama 12.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live