Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yabadili malengo Klabu Bingwa Afrika, Hersi afunguka

Eng. Hersi Yanga Meeting Yanga yabadili malengo Klabu Bingwa Afrika, Hersi afunguka

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa timu yao imekwenda kwenye hatua ya Makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, si kwa bahati mbaya bali ni kutokana na mipango waliyoiweka hivyo wanauhakika baada ya kuweka malengo ya awali ya kutinga makundi kwa sasa wanaweza kufikiria hatua ya mbele zaidi.

Hersi amesema kuwa Yanga inakwenda kupambana kwenye michuano hiyo ili kufikia hatua kubwa na kuweka alama na heshima na si kushiriki tu kama ambavyo vilabu vingi vimekuwa vikifanya.

“Kwa kuwa hatukuwa tumefika kwenye hatua ya makundi kwa muda mrefu, malengo yetu madogo ilikuwa ni kufika makundi na tunamshukuru Mungu tumeshafika. Kinachofuata sasa hivi ni kuset malengo mengine ya pili sasa.

“Katika uhalisia katika timu nne zinazoshiriki hatua ya makundi, uwezekano wa Yanga kuwa katika timu mbili za juu na kuingia kwenye hatua ya robo fainali upo, hayo ndiyo malengo yetu ambayo tunayaweka sasa hivi.

“Kwa hiyo katika timu nne za makundi sisi tupate nafasi mbili za juu zitakazotupa nafasi ya kwenda robo fainali, hayo ndiyo malengo yetu ya sasa,” amesema Eng. Hersi.

Hapo awali, Yanga iliweka malengo ya kutinga hatua ya makundi ya CAFCL jambo ambalo tayari wameshatimiza hivyo wanawaza kuingia robo fainali kisha watapiga hesabu zao nyingine huko mbele ya safari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live