Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yabadili gia angani dili la Sowah

Balekeee Simbas.jpeg Yanga yabadili gia angani dili la Sowah

Sun, 7 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna uwezekano mkubwa Yanga ikamsajili mshambuliaji Jean Baleke na kuachana na mpango wa kumsajili Jonathan Sowah.

Baleke yuko nchini tangu wiki iliyopita ambapo taarifa za uhakika ni kuwa Yanga imefanya mazungumzo nae na kukubaliana masuala binafsi.

Hata hivyo bado mchezaji huyo ni mali ya TP Mazembe hivyo mabosi wanapambana kumalizana na Mazembe.

Sowah alikuwa katika nafasi nzuri ya kutua Yanga lakini ni wazi kile kilichotokea kwa Hafiz Konkoni na Augustine Okrah kimewapa hofu viongozi wa Yanga juu ya kusajili mchezaji mwingine kutoka Ghana.

Baleke aliitumikia Simba kwa mmoja kabla ya kuelekea Libya alikotolewa kwa mkopo na klabu yake ya TP Mazembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live