Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yabadili gia Algeria

Yanga Algeriaaaaaa Yanga yabadili gia Algeria

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kundi la kwanza la kikosi cha Yanga limewasili jana nchini Algeria tayari kuwavaana CR Belouizdad lakini mabosi wao wakabadili akili ya haraka kurudi hoteli yao ya bahati.

Yanga ilikuwa ifikie hoteli moja ya kisasa yenye hadhi ya nyota nne lakini wakashtuka na kubadili upepo ghafla na kurudi kutumia hoteli nyingine yenye hadhi kama hiyo ya Legacy Luxury.

Legacy Luxury ipo jiji la Algiers ambako Yanga itatua hapo na kucheza mchezo wao huo wa kwanza wa hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na wamefanya hivyo huku wenyeji wao wakijua kwamba watafikia kwenye hoteli waliyoikacha.

Yanga iliwahi kuweka kambi hoteli hiyo msimu uliopita walipokutana na USM Alger katika mchezo wa marudiano ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika waliposhinda kwa bao 1-0 Juni 3, 2023.

Mabingwa hao wanaona kama hoteli hiyo ni ya bahati kwao waliposhinda ugenini dhidi ya USM Alger ambao ndio timu inayosadikika kuwa na mashabiki wengi watukutu nchini humo.

Yanga wanaona kwamba watakuwa salama wakiwa hapo kwa kuwa mara ya mwisho licha ya vurugu kubwa ambazo walifanyiwa usiku na mashabiki wa USM Alger timu yao ilibaki salama.

Hata hivyo, CR Belouizdad wao sio timu yenye mashabiki wengi na wenye utukutu kulinganisha na USM Alger lakini mabosi wa Yanga wameweka tahadhari kubwa ya mapema.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) liliwalima barua kali shirikisho la soka nchini humo kutokana na vurugu dhidi ya Yanga ikiwemo kupiga fataki kali na sasa wametakiwa kuhakikisha matukio hayo hayajirudii kwenye mechi hizo.

Vurugu hizo za awali nusura zisababishe madhara makubwa kwa mratibu wa Yanga Hafidh Salehe ambaye Mwanaspoti linafahamu zilimletea madhara makubwa kiafya kiasi cha kupumzishwa wakati timu hiyo ikicheza na USM Alger.

CAF ndio waliosimamia matibabu ya Hafidh wakati huo kisha wao wakamalizana na USM kwa kuwalima faini kali za fedha.

Kuhusu utaratibu wa mastaa wote kufika kwa wakati, Rodgers Gumbo, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga ameliambia Mwanaspoti kuwa;”Tumeandaa utaratibu mzuri ndani na nje ya Uwanja.”

Anasema kwamba walijua ratiba hiyo na ndio maana wakatumia akili kuhakikisha kwamba kila mchezaji anafika Algeria kwa wakati na hata mawasiliano ni mazuri na timu za Taifa wakielewa umuhimu wa mchezo huo.

Chanzo: Mwanaspoti