Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaanza mikakati ya ushindi Sudan, wawili watangulizwa

FAD8084F D046 4E44 8143 67B3A73A102D.jpeg Viongozi Yanga wamewasili Sudan kuanza maandalizi

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi wa Yanga wanajipanga kwa mchezo wa marudiano dhidi ya Al Hilal na jana Jumatatu wameondoka vigogo wawili kwenda Sudan tayari kwa maandalizi ya awali kabla ya timu hiyo kusafiri baadaye wiki hii.

Yanga inawatanguliza mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh pamoja na kigogo mwingine wa Kamati ya Mashindano ya Klabu ili kuweka mambo sawa kwa maandalizi kabla ya mchezo huo ambao timu hiyo inahitaji ushindi wa aina yoyote ama sare inayozidi bao moja ili irejee rekodi ya mwaka 1998 ilipocheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akiongea kocha mkuu wa timu hiyo Nasreddine Nabi alisema Yanga haitakwenda kinyonge jijini humo na wala hawatakwenda na mbinu za kujilinda katika mchezo huo ambao utapigwa Jumapili.

“Kuna sehemu tulifanya makosa sana ya kutotumia nafasi ambazo tulizitengeneza, tulicheza vizuri sana kipindi cha kwanza hasa dakika 55 za kwanza, tuliporuhusu goli hatukuonyesha ukomavu, tulinyon g’onyea sana,” alisema Nabi na kuongeza;

“Tunajua makosa yetu pia tunafahamu mashabiki wetu wameumia sana, huu ndio mchezo wa soka, hatujakata tamaa na wala hatutakwenda kurudiana nao tukiwa na akili ya kujilinda. Tutakwenda kuipigania Yanga, hii ni vita ya soka bado haijaisha tutazungumza na wachezaji kubadilisha muelekeo wa akili yao.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live