Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaanza maandalizi ya kuipa dozi Ihefu

Yanga Pacome Gamondi Zdc Yanga yaanza maandalizi ya kuipa dozi Ihefu

Thu, 16 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo wetu wa nusu fainali ya CRDB Confederation Cup dhidi ya Ihefu, kikosi cha Yanga kimeanza maandalizi kuhakikisha tunaibuka na ushindi na kufuzu fainali.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumapili ya wiki hii Mei 19, 2024 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Meneja wa Young Africans, Walter Harrson amezungumzia hali ya kikosi akisema wachezaji wote wapo vizuri na wameanza mazoezi kuelekea kutimiza lengo lingine la kutetea ubingwa wa michuano hiyo baada ya kutoka kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC.

“Habari Wananchi, Dar es Salaam ndiyo mahali ambapo timu ya Wananchi ipo kwa sasa hivi.

“Baada ya kutwaa ubingwa pale Manungu Complex, timu ya Wananchi imerejea mazoezini leo kuendelea na maandalizi ya mchezo wa nusu fainali ya CRDB Federation Cup dhidi ya Ihefu siku ya tarehe 19 pale kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

“Wananchi timu yenu ipo vizuri sana, tunashukuru sana kwa sapoti ambayo tumeipata pale Morogoro Manungu Complex dhidi ya Mtibwa, hakika mmeonyesha jinsi gani mnaweza mkawa mchezaji wa 12 katika kuhakikisha kwamba tunayapata matokeo. Timu ilivyorejea kipindi cha pili namna sapoti tuliyoipata ilituwezesha kabisa kuhakikisha kwamba tunapata pointi tatu ambazo zilitupelekea kutangaza ubingwa wetu wa 30 pale Manungu Complex Morogoro.

“Timu inaendelea na mazoezi hapa tukijiwinda na mchezo wetu wa nusu fainali dhidi ya Ihefu, kila kitu kipo sawa, kikosi kizima cha wachezaji wote wa Young Africans wako sawa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo muhimu ambao unatupelekea sasa kwenda kwenye malengo mengine ambayo tumejiwekea. Tunataka kutimiza malengo yote ya kuhakikisha vikombe vyote vinakuja Young Africans timu ya Wananchi.

“Mashabiki wa Arusha, mashabiki wa mikoa ya jirani na Arusha tunawakaribisha sana kama ambavyo imekuwa kawaida yenu mkitupa sapoti kuanzia tunapofika airport mpaka siku ya mchezo na hata baada ya mchezo.

“Nafasi imefika sasa tunatakiwa kuhakikisha tunakuwa nyuma ya timu yetu katika kuandika historia nyingine pale mkoani Arusha.

“Ni tarehe 19 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid karibuni sana kuhakikisha kwamba mnatupa sapoti ya kuelekea sasa hatua ya fainali kwenda kutimiza lengo lingine ambalo Young Africans tumejiwekea msimu huu. Karibuni sana Arusha, tupo vizuri na tunakuja kuwapa furaha,” alisema Harsson.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live