Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaanza kuandaa tano tano nyingine za msimu ujao

Yangasc Coco Yanga yaanza kuandaa tano tano nyingine za msimu ujao

Thu, 11 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jana jioni kikosi cha Young Africans SC kilifanya mazoezi katika Ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam.

Mazoezi hayo ni sehemu ya program chini ya benchi la ufundi linaloongozwa na Miguel Gamondi ambaye alikuwepo mazoezini akionekana kufurahia alipokutana tena na vijana wake.

Wachezaji wote wapya waliotambulishwa hivi karibuni wamehudhuria mazoezi hayo akiwemo Clatous Chama, Chadrack Boka na Prince Dube.

Mbali na wachezaji wapya, pia wale wa zamani waliokuwa na kikosi kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC na Kombe la Shirikisho la CRDB Bank wakiongozwa na nahodha, Bakari Mwamnyeto nao walikuwepo.

Program ya jana ilikuwa ni siku ya tatu ya mazoezi baada ya kuanza maandalizi yetu juzi Jumatatu Julai 8, 2024.

Mazoezi ya siku mbili yaliyopita Jumatatu na juzi Jumanne yalikuwa ni katika gym huku jana yakifanyikwa ufukweni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live