Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaanza Ligi kwa kuichapa Kagera Sugar

Yanga Kagera 0001 Yanga yaanza Ligi kwa kuichapa Kagera Sugar

Fri, 30 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Young Africans Sports Club wameanza utetezi wa ubingwa huo kwa msimu wa 2024/2025 baada ya kuwachapa Kagera Sugar mabao 2-0.

Kagera Sugar iliwaalika Yanga SC kwenye uwanja wa Kaitaba saa 11:00 jioni ya Agosti 29, 2024 ukiwa ni mchezo wa pili kwao na wa kwanza kwa wageni hao.

Ni baada ya Yanga SC kurejea kutoka kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika ambapo katika hatua za awali imevuna alama sita na mabao 10 dhidi ya Vital’OyaBurundi na kusonga mbele katika hatua ya pili ya mtoano.

Dakika ya 26 ya kipindi cha kwanza, Maxi Mpia Nzengeli alianza kulipa bili ya mwajiri wake kwa kutupia bao safi ambalo lilidumu hadi mapumziko.

Licha ya Yanga SC,kuwa na nafasi ya kupata mabao mengi zaidi kupitia mtanange huo, mambo hayakwenda vema, lakini Clement Mzize dakika ya 88 aliongeza bao la pili dakika za jioni.

Hadi mtanange huo unafikia tamati, ubao ulikuwa unasoma mabao 2-0, hivyo kuifanya Yanga SC kuanza vema safari yao katika ligi hiyo yenye timu 16.

FT: Kagera Sugar 0-2 Yanga Sc

⚽ Maxi 26'

⚽ Mzize 88'

NB: Ubao ungesomeka tofauti kama sio zile kosa kosa za Prince Dube.

KMC vs Coastal Union

Mchezo wa kwanza ulipigwa saa 10:00 Alasiri kati yaKMC na Coastal Union kwenye uwanja wa KMCComplex, Dar es Salaam.

Aidha,mchezo huo ni wa kwanza kwa timu zote mbilikatika msimu huu ambapo dakika ya 33,lbrahim llyasAhmed alianza kuiandikia KMC bao la kwanza.

Ni bao ambalo lilidumu mpaka kipindi cha pili dakika ya86 ambapo Maabad Maulid alisawazisha, hivyo haditamati ubao ukasoma sare ya bao 1-1.

Namungo FC vs Fountain Gate FC

Katika mchezo wa mwisho uliozikutanisha Namungo FC dhidi ya Fountain Gate FC katika Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi, wenyeji wamekubali kichapo cha mabao 2-0.

Mchezo huu ulitakiwa kuchezwa hapo awali, lakini uliahirishwa baada ya Fountain Gate kuwa na changamoto za usajili.

Aidha, matokeo hayo yanaifanya Namungo FC kuwa na mwanzo usioridhisha kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, baada ya awali kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka Tabora United FC.

Mabao ya Fountain Gate FC yamefungwa na Edgar William dakika ya 30' huku dakika ya 45, Seleman Mwalimu akifunga hesabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live