Baada ya utambulisho wa Nickson Kibabage, ikapita wiki nzima pasipo Yanga kutambulisha mchezaji mwingine kabla ya jana jioni kumshusha beki kisiki Gift Fred
Presha ilikuwa juu miongoni mwa mashabiki na Wanachama wa Yanga ambao baadhi yao walianza kuamini yale yaliyokuwa yakiandikwa mitandaoni
Utambulisho wa Gift umedhaminiwa na Benki ya CRDB na umetoa majibu kwa nini Yanga ilichelewa kutoa taarifa za usajili wake
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amefafanua kuwa ulikuwa mkakati wa kibiashara ambao umeifanya Yanga kuwa klabu ya kwanza kuwa utambulisho wa wachezaji wake wapya kudhaminiwa (pesa imeingia klabuni)
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Kamwe ametoa ufafanuzi huu
"Kwanini Yanga imechelewa kutambulisha wachezaji? Swali jepesi kutoka mtaani na baadae ikawa Topic nzito kwenye vyombo vya Habari.
Waandishi wakaandika. Wachambuzi wakazungumza. Presha ikapanda kwenye mioyo ya mashabiki na baadhi wakaanza kuamini kwenye ‘Uzushi’.
Mara Yanga imefungiwa kusajili.. Mara viongozi hawana hela .. Blaah Blaah zikawa nyingi.
Lakini leo, kupitia utambulisho wa GIFT FRED MAJIBU YAMEPATIKANA.
Utambulisho wa wachezaji ni Content yenye Thamani kubwa sana. Uhitaji wake hufanya watu kukesha, kukopa fedha kulipia/kutafuta habari sahihi inapopatikana.
This Time YANGA tukasema Hapana. Let’s Try kitu kipya. Thamani hii tuigeuze kuwa Fedha kwa Klabu yetu.
Ni kama ambavyo wachambuzi husema, wachezaji flani flani Ulaya usajili wao ulilipa siku ya kwanza baada ya kutambulishwa.. Kwanini Hilo lisifanyike hapa Tanzania?
Kwa Msisimko huu wa Football ya Tanzania kwenye mitandao ya Kijamii, kwanini hii isiwe sehemu ya pato la klabu?
Idara za wachapakazi wa Yanga SC zikaingia kazini. Demand ikatengenezwa sokoni, miswada ikaandaliwa na kusambazwa kwenye Makampuni na hatimaye, BENKI YA CRDB wakabeba Package hii ya Udhamini wa utambulisho wa Wachezaji wetu Msimu huu.
Football ni Biashara Mabibi na Mabwana.. Na Uongozi huu wa Yanga chini ya Rais Hersi Said unataka kushinda uwanjani na kushinda kwenye akaunti zetu za Benki
Mambo mazuri zaidi Yanakuja Wananchi."