Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaangukia pua rufaa ya Aucho TFF

Aucho X Aziz KI Yanga yaangukia pua rufaa ya Aucho TFF

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi kuu Bara imejadili maombi ya marejeo (review)ya klabu ya Yanga kuhusu adhabu ya kufungiwa michezo mitatu 3 na kutozwa faini ya Sh500,000 iliyotolewa kwa mchezaji Khalidi Aucho kupiti kikao cha kamati hiyo Novemba 14, 2023.

Aucho alikumbana na kibano hicho kutokana na kosa la kumpiga kiwiko nahodha wa Coastal Union, Ibrahim Ajibu katika mchezo namba 71 uliopigwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Hata hivyo baada ya kupitia maelekezo ya klabu ya Yanga na kanuni nza Ligi kamati imejiridhisha kwa mara nyingine kuwa adhabu iliyotolewa kwa mchezaji huyo ni sahaihi hivyo anapaswa kuendelea kuitumikia huku ikimtaka mchezaji huyo kuzingatia michezo ya kiungwana wakati wote.

Yanga ilikata rufaa siku moja baada ya Kamati ya Kusimamia na Kuendesha Ligi ya Bodi ya Ligi (TPLB) kutangaza kumfungia kiungo wa Yanga, Khalid Aucho kwa mechi tatu na kumlima faini ya Sh500,000 kwa kosa la utovu wa nidhamu.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: