Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaandika rekodi kwa Namungo

Yanga Ft 2 1 Kikosi cha Yanga kilichoanza mchezo vs Namungo

Sat, 23 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye Yanga imepata ushindi wa kwanza Ligi Kuu dhidi ya Namungo baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa usiku huu.

Magoli ya Yanga katika mchezo wa leo yamefunga na Fiston Mayele na Feisal Salum kipindi cha kwanza huku lile la Namungo likifungwa na Shiza Kichuya nalo pia kipindi cha kwanza.

Kabla ya mchezo wa Leo, Yanga na Namungo wamekutana mara tano na zote zikimalizika kwa sare.

Hivyo ushindi wa Yanga leo ndio ushindi wa kwanza mechi za Ligi tangu kupanda kwa timu ya Namungo msimu wa 2020/2021.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live