Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaandamwa na majeruhi, daktari afunguka

Bacca Mwamnyeto Sure Boy Yanga A0006 Yanga yaandamwa na majeruhi, daktari afunguka

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Daktari wa kikosi cha Yanga, Moses Etutu ametoa ripoti ya wachezaji wq timu hiyo ambao ni majeruhi kuelekea mchezo wa Ligi KuuBara dhidi ya DodomaJiji utakaopigwa leo pale Azam Complex Chamazi.

Sure Boy

Kiungo Salum Abubarak ‘Sure Boy’ aliyeumia mkono kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar, leo atapelekwa hospitali kwa ajili ya vipimo zaidi juu ya jeraha lake.

Taarifa ya awali inaonyesha kuwa kiungo huyo atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki 2, lakini kama vipimo vitaonyesha jeraha ni kubwa zaidi basi Sure Boy anaweza kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu zaidi.

Ibrahim Hamad Bacca Beki huyu wa kati ataendelea kuwa nje ya uwanja wa siku 5 baada ya kupata jeraha la enka akiwa kwenye majukumu ya Timu ya Taifa.

Kwa Taarifa hii, Bacca atakuwa nje ya kikosi cha Yanga kitakachocheza dhidi ya Dodoma Jiji, utakaochezwa Azam Complex Leo majira ya saa 1:00 jioni.

Bakari Mwamnyeto

Nahodha wetu Bakari Mwamnyeto alipata majeraha pia akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa atakuokosa mchezo wa leo dhidi ya Dodoma Jiji kwa sababu ya mejeraha yake ya paja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live