Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaandaa mkataba mnono kwa Aziz Ki

Ki Aziz.jpeg Aziz Ki

Sat, 23 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa Asec Mimosas, Stephane Aziz Ki, raia wa Burkina Faso.

Hiyo ni katika kukiboresha kikosi chao ambacho msimu ujao kitacheza Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga inadaiwa hadi hivi sasa tayari imefanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji wa timu ya taifa ya Burundi na Klabu ya Kiyovu ya Rwanda, Abedi Bigirimana.

Inaelezwa kuwa kiungo huyo amesajiliwa kwa dau la Sh 200Mil ambaye anatarajiwa kutambulishwa mwishoni mwa msimu huu.

Mmoja wa mabosi wa Yanga, amesema kuwa yapo mazungumzo yanayoendelea kufanyika kati ya menejimenti ya kiungo huyo na mmoja wa viongozi wakubwa wenye ushawishi wa usajili wa Jangwani.

Bosi huyo alisema kuwa mazungumzo yanaendelea vizuri kati ya klabu yake anayoichezea ya Asec na Yanga katika kufanikisha dili hilo la usajili unaotajwa utakuwa wa gharama kubwa kama dili hilo litakamilika kwa haraka.

Aliongeza kuwa kiungo huyo mwenyewe ameonyesha nia kubwa ya kusajiliwa na Yanga kutokana na ukubwa wa timu ilionao, pia dau la usajili ambalo amewekewa mezani ili akubali kusaini.

“Aziz ni kati ya wachezaji bora, hivyo anahitajika katika timu yenye malengo ya kufanya vizuri ikiwemo kuchukua makombe hasa kimataifa zaidi.

“Hivyo yapo mazungumzo yanayoendelea hivi sasa na wachezaji baadhi wa kigeni wenye uwezo na uzoefu wa kucheza michuano ya kimataifa, akiwemo Aziz.

“Mazungumzo hayo yamefikia pazuri na kama mambo yakienda vizuri, atakuwa sehemu ya wachezaji wetu katika msimu ujao ambao tunakwenda kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema bosi huyo.

Akizungumzia usajili, Mjumbe wa Kamati ya Mashindano na Usajili ya Yanga, Injinia Hersi alisema: “Katika kuelekea msimu ujao, tumepanga kufanya usajili wenye thamani kubwa Afrika.

“Usajili huo unakwenda kuitangaza kimataifa Yanga ambayo msimu ujao tunakwenda kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo ni lazima tuwe na timu bora itakayoleta ushindani.”

Akizungumzia juu ya usajili wa Aziz, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema mashabiki wa timu hiyo wanatakiwa kuwa watulivu kwani watafanya usajili wa maana.

“Watu wanatakiwa kukaa kwa kutulia kwani mambo ya usajili bado hayajafikia wakati wake sahihi, kwa sasa tunaangalia zaidi michezo yetu inayofuata ya ligi kuu na ukifika muda wa usajili basi mashabiki wa Yanga watafahamu kama tumemsajili Aziz Ki au la.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live