Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaaga mashindano CAF

Timu Boraaas Yanga yaaga mashindano CAF

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hii ndio orodha ya Mwisho ya vilabu vitatu vitakavyowania Tuzo ya CAF AWARDS 2023 CLUB OF THE YEAR iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF)

TOP THREE [3] YA KLABU BORA YA 2023 CAF

Al Ahly SC (Misri) - Bingwa wa Ligi ya mabingwa Afrika [2022/23], Finalist wa CAF Super Cup 2023].

Wydad AC (Morocco) - Finalist wa Ligi ya mabingwa Afrika [2023/24], Finalist wa AFL [2023].

Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) - Bingwa wa AFL [2023].

Klabu ya Soka ya Young Africans (Yanga SC) ilikuwa kwenye orodha ya 5 bora ya vilabu vilivyokuwa vikiwania tuzo hiyo pamoja na USM Alger ya Algeria lakini timu hizo mbili zimeondolewa katika king'anyiro hicho.

Yanga and USM Alger walicheza fainali ya CAF Confederation Cup (CAF CC) ambapo USM Alger walishinda Ubingwa huo kwa kanuni ya bao la ugenini baada ya kutoka sare ya bao 2-2 kwenye michezo miwili.

Al Ahly alicheza na Wydad Casablanca kwenye fainali ya CAF Champions League ambapo Ahly alichukua Ubingwa huo kwa ushindi wa mabao 2-1.

Mamelodi Sundowns, ndiyo mabingwa wapya wa michuano mipya ya Africa Football League (AFL) 2023.

USM Alger ametoka kwenye orodha ya timu tatu, ikiwa ni Bingwa wa CAFCC [2022/23] na Bingwa wa CAF Super Cup [2023].

Chanzo: www.tanzaniaweb.live