Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaacha watano Dar

Balama Pic Yanga yaacha watano Dar

Wed, 4 May 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Baada ya suluhu dhidi ya watani zao Simba, Yanga leo saa 10 jioni itakuwa uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma kuivaa Ruvu Shooting wakiwa na mastaa wao 20 huku wakiwaacha watano jijini Dar es Salaam.

Walioachwa Dar ni Deus Kaseke, David Bryson, Chico Ushindi, Yacoub Sogne, Balama Mapinduzi, Paul Godfrey na Yusuf Athuman.

Mastaa waliopo Kigoma kwa ajili ya mchezo huo muhimu wa Ligi Kuu ni Djigui Diarra, Shaban Djuma, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Kibwana Shomari, Khalid Aucho, Yanick Bangala, Feisal Salum, Said Ntibazonkiza, Jesus Mayele na Fiston Mayele.

Wengine ni Abdultwalib Mshery, Erick Johora, Yassin Mustafa, Ibrahim Bacca, Abdallah Shaib, Zawadi Mauya, Salum Abubakari, Farid Mussa, Denis Nkane, Chrispin Ngushi na Haritier Makambo.

Kocha msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze alisema wamesafiri na wachezaji wote kwa sababu wanafahamu umuhimu wa mechi wanayocheza huku akiweka wazi kuwa walioachwa hawapo fiti.

“Kikosi chote kilichocheza na Simba kuanzia waliocheza na waliokaa benchi pia tumeongeza wawili kukamilisha idadi ya wachezaji 20 lengo ni kuona tunakuwa na kikosi kipana ambacho kitatimiza lengo la pointi tatu bila kujali uwanja,” alisema.

Kaze alisema bado wanahitaji ushindi kwenye kila mchezo na hawana sababu za kuwapumzisha baadhi ya wachezaji watatumika kama kawaida, lengo ni kuona wanacheza kwa umoja na kufikia malengo ya kutwaa taji kwa kuwaacha pointi nyingi wanaowakimbiza.

“Uwepo wa mastaa wetu wote ni moja ya hamasa kwa mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi kuja kuwashuihudia na kuwapa nguvu kwa ajili ya kuhamasisha ushindi.”

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz