Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wembe uleule Manungu, Aziz Ki azua gumzo

Aziz Ki Goal Manungu Stephen Aziz Ki, mfungaji wa bao pekee la Yanga

Sat, 31 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi, Yanga SC wameuga mwaka 2022 kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 26.

Kwa ushindi huo, Yanga SC wanafikisha pointi 50 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi ya watani, Simba baada ya wote kucheza mechi 19.

Kwa upande wao, Mtibwa Sugar baada ya kipigo hicho wanabaki na pointi zao 24 za mechi 19 nafasi ya nane.

Bao hilo la pekee katika mcezo huo limeendeleza lawama kwa magolikipa huku wengi wao wakionekana wanafungwa kutokana na uzembe.

Lakini upande mwingine kuna wanaodai sio rahisi kukamata mipira inayopigwa na nyota huyo wa Yanga na wakidai apewe sifa zake kwa umahiri anaoonesha katika upigaji wa mipira ya adhabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live