Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wazitaka alama tatu Azam FC

Yanga V Azam 640x424 Wachezaji wa Yanga walimkabili kiungo wa Azam FC

Thu, 1 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga kipo kwenye maandalizi ya mchezo wao wa ligi ujao dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Septemba 6,2022 Uwanja wa Mkapa.

Timu hiyo inanolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ambaye ameongoza kwenye mechi mbili za ligi bila kuonja ladha ya kupoteza.

Akizungumza na waandishi wa habari kocha Nabi ameweka wazi kuwa mchezo huo utakuwa mgumu ila wapo tayari kwa ajili ya kusaka matokeo ndni ya daika 90.

“Tunatambua kwamba kila mechi ni ngumu na ushindani kwenye ligi ni mkubwa hivyo tutajitahidi kupata ushindi kwa ajili ya kuzidi kuwa imara zaidi kupambania taji la ligi na kufikia malengo ambayo tumejiwekea,” amesema.

Kwa upande wa Azam FC, Ofisa Habari wa timu hiyo Zakaria Thabit amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo watajitahidi kupambana kupata ushindi.

“Maandalizi yanaendelea na tupo tayari kwa ajili ya mechi zote wachezaji wapo tayari,” amesema.

Azam FC imepata ushindi kwenye mechi moja na kulazimisha sare kwenye mchezo mmoja wa ligi msimu wa 2022/23.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live