Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wawafuata Mashujaa kibabe Kigoma

Yanga Wawafuata Mashujaa Kigoma Yanga wawafuata Mashujaa kibabe Kigoma

Sat, 4 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga SC kimeianza safari ya kuelekea mkoani Kigoma kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mashujaa FC utakaopigwa kesho Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani humo.

Jeshi hilo la kijani na njano lipo katika hesabu kali za kutaka kuutetea ubingwa wa ligi kwa mara ya tatu baada ya kutwaa misimu miwili iliyopita.

Mpaka sasa wababe hao wa mitaa ya Twiga na Jangwani wamejikusanyia alama 62 kwenye michezo 24 waliyoshuka dimbani msimu huu.

Wenyeji wa mchezo huo Mashujaa FC wanapigana na vita ya kushuka daraja wakiwa nafasi ya 14 na alama zao 23 baada ya michezo 24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live