Baada ya jana kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 ugenini dhidi ya Namungo FC, kikosi cha timu ya Young Africans SC kimerejea Dar es Salaam leo Jumamosi kikitokea Ruangwa mkoani Lindi.
Baada ya kurejea Dar es Salaam, programu ya mazoezi imeanza kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Jumatatu dhidi ya Ihefu.
Wachezaji ambao leo wana program ya mazoezi ni wale waliocheza dakika chache mechi ya jana na waliokosa nafasi kabisa. Program hiyo ya leo ni ya gym ambapo inafanyika Gymkhana.
Kesho Jumapili, mazoezi yatafanyika Avic Town yakihusisha wachezaji wote, ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC tutakaoucheza Jumatatu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 12:00 jioni.