Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga watua Dar kuwawinda Simba

Yanga Dar Sdv Yanga watua Dar kuwawinda Simba

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha timu ya Young Africans SC, kimerejea Dar es Salaam kikitokea Mwanza, baada ya kukusanya alama tatu katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa jana Jumapili.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Young Africans SC iliibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya wenyeji wetu, Singida Fountain Gate.

Baada ya kurejea Dar es Salaam, kikosi moja kwa moja kinaanza maandalizi ya kuelekea mchezo ujao wa Kariakoo Dabi ndani ya Ligi Kuu ya NBC.

Kariakoo Dabi ambayo itachezwa Jumamosi ya wiki hii kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 11:00 jioni, Yanga itaingia uwanjani ikiwa inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC kwa pointi 55.

Ikumbukwe kwamba, katika Kariakoo Dabi ya mzunguko wa kwanza, Yanga waliibuka na ushindi wa magoli 5-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live