Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga watoka patupu Kombe la Shirikisho Afrika, USM Algiers wabeba Ubingwa

IMG 4233 USM Algiers.jpeg USM Algiers mabingwa wapya Kombe la Shirikisho Afrika

Sat, 3 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Timu ya Yanga imetoka patupu katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya USM Algiers kutoka nchini Algeria.

Yanga ilipoteza mchezo mkondo wa kwanza wa Fainali uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kwa mabao 2-1.

Mchezo huo wa Fainali ya pili uliopigwa katika Uwanja Julai 5 nchini Algeria uliwashuhudia Yanga wakionesha kiwango safi na kupata bao dakika ya 7 tu ya mchezo likiwekwa kimiani na Mlinzi Djuma Shaban.

Mpaka dakika 90 zinakamilika matokeo ya Jumla yalikuwa 2-2 lakini USM Algiers wamebeba Ubingwa kwa faida ya goli la ugenini ambako walipata mabao mawili ugenini.

Mlinda mlango wa Yanga, Djigui Diarra ndio alieibuka nyota wa mchezo kutokana na kazi nzuri aliyofanya langoni mwa Yanga.

Hii ni mara ya kwanza kwa USM Algiers kubeba Ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika na kuweka rekodi kwa klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: