Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga watoa ahadi nzito Kimataifa

Yanga Ahadi Kimataifa Yanga watoa ahadi nzito Kimataifa

Mon, 27 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Haji amewatoa hofu na kuwahamasisha mashabiki wa timu hiyo na kuwatoa hofu ya matokeo ya mchezo wa jana dhidi ya Bamako uliomalizika kwa sare ya 1-1.

Arafat amesema matokeo ya jana hayakuwa mabaya na makocha wamekwisha kujua ni wapi walikosea katika mchezo huo na watarekebisha lakini pia zipo changamoto ambazo zilitokea kule ila wachezaji na uongozi pekee ndio wanazifahamu.

"Mashabiki endeleeni kuwa upande wa timu yenu kwani tunakikosi bora mnajua lakini msiingie kwenye mtego wa kutengenezewa hasira na wasiotupenda kwani hakuna timu msimu huu inayoweza kutubeza,"

"Tuwape wachezaji wetu nafasi yao ya kujirekebisha wakati na sisi viongozi tukitekeleza wajibu wetu nanyi mkitekeleza wajibu wenu bado tunanafasi ya kushinda twendeni Machi 8 tukaendeleze furaha yetu."

Yanga iko njiani kurudi na watakapofika wataendelea na maandalizi mechi yao ya marudiano Machi 8 dhidi ya Real Bamako katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live