Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga watinga makundi Shirikisho Afrika

Yanga Makundi 1 0 Yanga imeibuka na ushindi wa goli 1-0, mfungaji akiwa ni Aziz Ki

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara Timu ya Yanga imetinga hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho barani Africa baada ya kuichapa bao 1-0 wenyeji club Africain mchezo uliopigwa nchini Tunisia.

Mchezo huo wa mkondo wa pili uliwashuhudia Yanga wakicheza katika kiwango bora baada ya ule wa awali kumalizika kwa sare Novemba 2 katika dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Shujaa wa Yanga ni kiungo mshambuliaji kutoka nchini Burkina faso akitokea benchi aliipatia bao muhimu timu yake dakika ya 79 Stephane Aziz Ki akimalizia pasi ya Fiston Mayele.

Kipigo hicho kilizua taharuki kwa wageni kwani baada ya filimbi ya mwamuzi kupulizwa kuashiria kutamatika kwa dakika 90, Mashabiki na baadhi ya wachezaji wa Club Africain waliansha vurugu kwa wachezaji wa Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live