Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wateka jukwaa la Simba mapema

69811 Simba+pic

Mon, 5 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MASHABIKI wa Yanga wameanza mbwembwe kwa kujaza jukwaa ambalo hukaliwa na mashabiki wa Simba kwenye michezo mbalimbali.

Simba ambao huanza kukaa upande wa kushoto wa jukwaa  Uwanja wa Taifa, lakini imeoneka tofauti kwa siku ya leo Jumapili wakati timu hiyo ikihitimisha Wiki ya Mwananchi itakapocheza mchezo wa kirafiki jioni dhidi ya Kariobangi Sharks ya Kenya.

Mashabiki wanaonekana kutawala upande huo ni pamoja na tawi la Yanga la Makumbusho Terminal, Kijitonyama Shule, Mashabiki kutoka Mkoa wa Geita, Morogoro, Ulongani na Tawi la Stop Over.

Rangi ya njano na kijani ndio imetawala zaidi Uwanja wa Taifa kwa mashabiki kufurahia kwa pamoja watakapowaona wachezaji wao watakaopeperusha Bendera msimu huu na mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Chanzo: mwananchi.co.tz