Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga watakuwa kama Man City

Chama Aziz Dube Yanga watakuwa kama Man City

Thu, 4 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia TV3, Boiboi Mkali amedai kuwa kwa usajili wanaoufanya Klabu ya Yanga, watatamba sana kwenye soka la Bongo kama ilivyo Man City pale Uingereza.

Boiboi amesema hayo baada ya Yanga kumsajili aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama huku kukiwa na tetesi za kumsajili mshambuliaji Prince Dube ambaye ameshavunja mkataba wake na Azam FC.

"Kama klabu zingine hazitoshtuka na kuanza kujitutumua misuli tunaweza kuja kuwa na ligi ambayo itatawaliwa na klabu Moja Kwa miaka mingi sana kama ambavyo ilivyo kule ufaransa Kwa PSG au pale Uingereza Kwa Man City.

"Yanga wanatengeneza kikosi ambacho kitakuwa hatari na tishio ndani na nje ya nchi, kikosi ambacho kitakuja kutawala ligi Kwa muda mrefu sana, ukikiangalia kikosi Chao Kwa Sasa utakubaliana na mimi kwamba Yanga wanaweza kuwa watawala Kwa muda mrefu," amesema Boiboi Mkali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live