Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wataikuta pesa yao Airport

Mwana Fa Yanga Er.jpeg Yanga wataikuta pesa yao Airport

Wed, 17 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ amewasihi Yanga kupambana ili kuliheshimisha Taifa kwa kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga leo watakuwa na kibarua mbele ya Marumo Gallants nchini Afrika Kusini katika mchezo wa pili wa nusu fainali ya michuano hiyo baada ya Yanga kushinda mchezo wa kwanza kwa bao 2-0.

“Huwezi kutapeliwa na Serikali, na inafahamika mama hana mbambamba, mimi nimekuja tu kushuhudia magoli yanafungwa kweli, halafu pesa yao wataikuta Airport bila wasiwasi. Nisingeweza kutembea na begi la pesa hizo, kwanza ningesema nazipeleka wapi?

“Serikali haiwezi kuwapiga changa la macho, kwa hiyo kila goli wanalofunga kuna Tsh milioni 10 ya mama, kwa sababu hatua ni kubwa, huwezi kujua mama ataamkaje huenda akaongeza vilevile.

“Nitashangaa kuona watu wanaiponda Yanga, hili ni suala la kitaifa na si Yanga pekee kwa vile inapeperusha bendera ya Taifa. Wale tuliofanikiwa kufika tuisapoti kwa nguvu zote na wale waliobaki nyumbani basi waiombee Yanga ishinde na kutinga Fainali,” amesema Mwana FA.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: