Klabu ya Yanga wamejihakikishia USD $900,000 sawa na Tsh bilioni 2.3 baada ya kutinga robo fainali CAF-CL.
Yanga SC wameongeza points (3) kwenye CAF Ranking, maana yake watasogea kutoka nafasi ya (18) hadi mbele. Miongoni mwa tofauti kati ya Yanga ya Nabi na ya Gamondi ni ukatili.
Msimu uliopita Yanga walishinda magoli (4+) kwenye mechi (1) katika michezo (3) tu. Msimu huu wameshinda Magoli (4+) kwenye mechi 1 katika michezo (9) mpaka sasa;
◉ 5 - 0 KMC
◉ 5 - 0 JKT Tanzania
◉ 5 - 1 ASAS Djibouti
◉ 5 - 1 Simba SC
◉ 4 - 1 Mtibwa sugar
◉ 5 - 0 Jamhuri
◉ 5 - 1 Housing FC
◉ 5 - 0 Polisi Tanzania
◉ 4 - 0 CR Belouizdad
4 — Timu zilizokuwa 'LOSER CUP' kama Wandewa walivyosema msimu uliopita zimefuzu robo fainali CAF champions league tena zikiwa na Mchezo mkononi.
Young Africans ☑️
ASEC Mimosas ☑️
TP Mazembe ☑️
Ukitazama mechi nyingi za CAF-CL msimu huu za timu ambazo zina nafasi kubwa ya kutinga robo fainali CAF-CL, Yanga wanavyocheza kwa sasa wanaweza kucheza na timu yoyote kati ya hizo na wakazitoa wakatinga nusu au hadi fainali.
Mfano, CR Belouizdad mabingwa wa Algeriamara nne mfululizo waliopigwa bao (4) na Yanga wamecheza mechi mbili msimu huu, Misrina Algeria dhidi ya Al-Ahly, Al-Ahly ambao ni mabingwa wa muda wote wa Africa hawakupata bao lolote dhidi ya Belouizdad na Al-Ahly walizidiwa kitakwimu.
Vinara wa mabao ya kufunga kwenye kundi (D) mpaka sasa CAF champions league;
1. ⚽ 9 — Young Africans
2. ⚽ 5 — Al-Ahly
3. ⚽ 4 — CR Belouizdad
4. ⚽ 3 — Medeama.
Timu zilizoifunga CR Belouizdad mabao (4) miaka ya karibuni CAF-CL ni ;
◉ Mamelodi 4 - 1 Belouizdad
◉ Yanga SC 4 - 0 Belouizdad.
Nini maana yake? Yanga kwa sasa wameanza kuwa tishio Africa, wasipuuzwe.