Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga warejea Dar kuiwinda KMC

Yanga Auchooo Yanga warejea Dar kuiwinda KMC

Tue, 13 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Young Africans SC, kimerejea Dar es Salaam jana Jumatatu kikitokea Mbeya baada ya jana Jumapili kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya wenyeji wetu, Tanzania Prisons, katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa Uwanja wa Sokoine jijini humo.

Baada ya kurejea Dar es Salaam, kikosi cha Young Africans SC sasa kinajiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC ukiwa ni mzunguko wa pili wa ligi hiyo.

Mchezo huo ambao watakuwa ugenini, umepangwa kuchezwa Jumamosi ya wiki hii Februari 17, 2024 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Ikumbukwe kwamba, Yanga ilipokutana na KMC katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, waliibuka na ushindi wa magoli 5-0, wafungaji wakiwa ni Dickson Job, Aziz Ki, Hafiz Konkoni, Mudathir Yahya na Pacome Zouzoua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: