Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga warejea Dar

YANGA MEK.jpeg Yanga warejea Dar

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Young Africans kimeanza safari mapema leo Jumatatu, Oktoba 17, 2022 asubuhi kurudi nyumbani ikitokea Sudan kupitia Ethiopia.

Yanga ilikuwa Sudan kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika na kukubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa wenyeji wao Al Hilal Omdurman katika mechi iliyochezwa Khartoum.

Kwa matokeo hayo, Yanga, ambao ni mabingwa wa Tanzania Bara wametolewa katika mashindano hayo makubwa barani Afrika kwa matokeo ya jumla (aggregate 2-1).

Hii ni kufuatia matokeo ya sare ya 1-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Goli pekee lililofungwa na Mohamed Abdelrahman katika dakika ya tatu ndio limewafungasha virago wawakilishi hao.

Hata hivyo, kuondoshwa kwa Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kunaifanya rasmi timu hiyo kuanguka katika kombe la Shirikisho ambapo sasa itacheza na timu moja kwenye hatua ya mchujo ili kusaka nafasi ya kutinga makundi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live