Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wapindua meza Azam FC, wapanga kuzoa wawili

Vita Vita Yanga Vs Azam Nyota wa Azam FC wanaowindwa na Yanga, kiungo James Akaminko pamoja na Kipre Jr

Wed, 28 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vita ni vita baina ya vigogo wawili. Klabu ya Yanga imetuma maombi rasmi hii leo kwenda klabu ya Azam FC kwa ajili ya kuwasajili kiungo James Akaminko pamoja na Kipre Jr.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kusambaa kwa taarifa za Kiungo nyota wa Yanga, Feisal Salum kuvunja mkatana wake na Yanga akitajwa kutaka kutimkia Azam FC.

Uongozi wa Azam FC kupitia kwa Kaimu Afisa Habari wake, Hasheem Ibwe umekiri kupokea maombi ya Yanga na kueleza kuwa bado kuna taratibu zinaendelea kufuatwa.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Ibwe ameandika;

"Azam fc inathibitisha kupokea Maombi Ya Yanga sc mapema leo juu ya uwezekano wa kunasa saini ya nyota wetu wawili JAMES AKAMINKO na KIPRE JUNIOR.

Maombi yamepokelewa na hivi karibuni watajibiwa kama wanapatikana au la! Na hiyo ni Baada ya Vikao vya ndani kufanyika pande zote 2".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live