Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wapigwa faini Mil. 5

KIKOSI CHA YANGAA Yanga wapigwa faini Mil. 5

Tue, 8 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Young Africans imetozwa faini ya Sh. 5,000,000 (milioni tano) kwa kosa la kuingia chumba cha kuvalia kupitia mlango usio rasmi kuelekea mchezo wao dhidi ya Mtani Simba SC uliofanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Oktoba 23, 2022.

Kwa mujibu wa Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Novemba 4, 2022 Adhabu hiyo ni kwa uzingativu wa Kanuni ya 17:(21 & 60) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Kwenye mchezo huo Yanga SC ilitoka sare ya goli 1 - 1 dhidi ya mtani wake wa jadi Simba SC uliyopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Oktoba 23, 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live