Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wapelekwa Uwanja wa nyumbani Algeria

Yanga ZtR.jpeg Yanga wapelekwa Uwanja wa nyumbani Algeria

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga itakipiga dhidi ya klabu ya CR Belouizdad Ijumaa hii 24 November 2023 katika uwanja wa Stade 5 Juillet 1962.

Kumbuka, Yanga SC walicheza fainali ya CAFCL katika uwanja huu dhidi ya klabu ya USM Alger ambayo ni miongoni mwa vilabu vyenye mashabiki wengi zaidi Nchini Algeria,

UWANJA: Uwanja ulijaa (Full-house), waliingia watazamaji takribani elfu sitini na sita (66).

Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1 , lakini wakashindwa kutwaa kombe kutokana na kanuni ya goli la ugenini.

Ijumaa hii wanarejea tena katika uwanja huo. Mchezo utachezwa saa 4:00 Usiku kwa saa za Afrika mashariki na saa 2:00 Usiku kwa saa za Nchini Algeria.

Kwa maana hiyo Yanga hawana ugeni na Uwanja huo na huenda wakaendeleza kile walichokifanya mara ya mwisho walipofika nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live