Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wanamtaka pacha wa Pacome na Aziz kuziba pengo la Mayele

Sankara Karamokoo 64087 Yanga wanamtaka pacha wa Pacome na Aziz kuziba pengo la Mayele

Sat, 11 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa za uhakika kutoka Yanga SC ni kwamba klabu hiyo inaufuatilia kwa karibu uongozi wa mshambuliaji Sankara William Karamoko (20) ili kupata saini yake katika dirisha lijalo la usajili.

Sankara raia wa Ivory Coast anahitajika Yanga ili kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji katika klabu hiyo na tayari wanajiandaa kutuma ofa, ni mshambuliaji mzuri sana.

Yanga wamerejea kwenye mchakato wa kusaka huduma ya mchezaji huyo baada ya kumkosa katika usajili uliopita ambapo mambo kadhaa hayakwenda sawa.

Iwapo Yanga watafanikiwa kumpata Sankara basi watakuwa wamelamba dume na kutengeneza partnership nzuri kwenye safu ya kiungo na ushambuliaji hasa ikizingatiwa kuwa amecheza pamoja na Aziz Ki na Pacome Zouzoua katika kikosi cha ASEC Mimosas.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live