Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wanaipa promo Simba SC - Oscar Oscar

Yanga A0011 Yanga wanaipa promo Simba SC - Oscar Oscar

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Ahmed Ally anaendelea zake na hamasa kwa ajili ya mchezo mkubwa wa African Football League (AFL) dhidi ya Al Ahly siku Ijumaa,ila Yanga nao wameongeza promo kuelekea mechi hiyo.

Kitendo cha mashabiki wa Yanga na baadhi ya maofisa wao kusema kwamba ni michuano ya majaribio ila kwa namna moja ama nyingine wanaendelea kuipa promo Simba kuelekea siku ya Ijumaa.

Wapo baadhi ya mashabiki wa Yanga wanaozungumza vibaya michuano hiyo ila kitendo chao kuzungumza kinaendelea kuwa faida kwa Simba na huku mashabiki wa Simba wakiendelea na ununuaji wa tiketi.

Ifike wakati Yanga wakubali kwamba Simba kushiriki michuano hii ya African Football League sio ndoto ya usingizi ila ni ile namna ya kuweka standard ya kufika hatua nyingi za Robo Fainali za CAFCL kitu ambacho Yanga wameshindwa kwa miaka 25 sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: