Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wanahitaji kocha wa wafungaji - Haatim

Haatim Mchambuzi.jpeg Yanga wanahitaji kocha wa wafungaji - Haatim

Mon, 21 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka, Haatim Abdul amesema Yanga SC wanahitaji mwalimu wa wafungaji kwani wanapata nafasi nyingi lakini wanashindwa kuzitumia.

Amesema, Yanga wanatakiwa kumtafuta mwalimu anayeweza kuwaelekeza mbinu za kufunga kwani kwa kiasi kikubwa wanafanya kila kitu kwenye mchezo lakini unakosekana umakini kwenye eneo la ufungaji.

"Wanamiliki vizuri mpira katikati, wanacheza kuanzia golini kwao lakini kule mwishoni bado kunakuwa na shida, wakati fulani Orlando Pirates walikuwa na tatizo kama hili, wakamtafuta kocha wa wafungaji wakamaliza tatizo hilo ndani ya muda mfupi," alisema Haatim.

Yanga jana walicheza na ASAS ya Djibouti mchezo wa hatua ya kwanza ya Klabu Bingwa Afrika na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 2-0 lakini walipoteza nafasi nyingi za wazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live