Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wanafurahisha kuwatazama

Young Squad Kikosi cha Yanga

Wed, 3 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni kama kila mtu anasubiri kwa hamu kubwa ili kuiona timu ya Yanga ikicheza uwanjani.

Soka la kuburudisha linalopigwa ama kuchezwa na kikosi hicho ndio kivutio kwa walio wengi.

Kila mmoja anataka aone leo Yanga wanacheza kwa staili gani, huku viungo wake watatu wakiwa ndio gumzo kila kona kwa sasa nchini, Khalidi Aucho, Yannick Bangala na Feisal Salum.

Wanacheza soka la kuburudisha, na wanapata matokeo, mchezo dhidi ya Ruvu Shooting Aucho hakucheza lakini bado Yanga walitandaza kabumbu Safi.

Nafasi ya Aucho aliikamata Mukoko Tonombe "Teacher" na wakaikamata show vile vile kila kona ya uwanja.

Katika ufungaji wa magoli yao kila siku wanazidi kuimarika, na kuboresha namna yao ya utafutaji wa magoli.

Walianza ligi kwa ushindi wa goli moja moja lakini mpaka mechi yao ya mwisho siku ya jana wameshinda magoli matatu dhidi ya Maafande wa Ruvu Shooting.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live