Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wanacheza kikubwa, hata ubingwa wa CAFCL watachukua

Yanga Mbg Yanga wanacheza kikubwa, wanaweza kuchukua ubingwa wa CAFCL

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Klabu ya Al Merreikh, Osama Nabih amesema Yanga SC inacheza kama vilabu vikubwa vya Ulaya na kubainisha kuwa hatashangaa ikiwa Yanga itatwaa ubingwa wa Afrika.

Al Merreikh imeondoshwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia kipigo cha jumla cha 3-0 dhidi ya Yanga kwenye hatua ya pili ya mtoano juzi Jumamosi, Septemba 30, 2023 katika Dimba la Azam Complex, Chamazi, Dar.

“Tumekutana na vilabu vikubwa vya Afrika, lakini tulivyocheza dhidi ya Yanga, tumeona ubora wao wa kipekee.

“Sitashangaa ikiwa Yanga itatwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu. Wanacheza kama vilabu vikubwa vya Ulaya," amesema Osama Nabih.

Msimu uliopita katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika na kufanikiwa kucheza fainali ambapo waliibuka washindi wa pili kwa kanuni ya bao la ugenini baada ya kutoa sare ya bao 2-2 na USM Alger ya Algeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: