Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wana shughuli nyingi kuliko kuzingatia matokeo - Edo Kumwembe

Yanga Supu 69148 Yanga wana shughuli nyingi kuliko kuzingatia matokeo - Edo Kumwembe

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi nguli wa masuala ya soka nchini, Edo Kumwembe amesema kuwa uongozi wa Klabu ya Yanga na mashabiki zao wamekuwa na shughuli nyingi za kusherehekea nje ya uwanja kuliko ku-deal na mechi zao ili wapate matokeo ndani ya uwanja.

Edo amesema hayo kufuatia Yanga kutopata matokeo mazuri kwenye michezo yake miwili ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa bao 3-0 na CR Belouizdad ya Algeria kisha sare 1-1 na Al Ahly.

Ikumbukwe kuwa, kabla ya mechi hizo Yanga walikuwa na sherehe ya kunywa supu Jangwani baada ya kuifunga Simba bao 5-1, harakati za kuweka mabango mabarabarani pamoja na sherehe nyingine waliowapa wazee wa Zanzibar ng'ombe wakati wakitangaza Bacca Day (siku maalum ya mchezi na Ahly).

“Kuna umuhimu kidogo wa Yanga kupunguza shughuli nyingi kabla ya mechi hizi. Yanga wana shughuli nyingi siyo kidogo. Mpaka kuna wakati unajiuliza kama wanazingatia kweli mechi au?” amesema Edo Kumwembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: