Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wana kazi kubwa kwa Namungo - Mchambuzi

Yanga Tizi Kigali Yanga wana kazi kubwa kwa Namungo - Mchambuzi

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka EA Radio na EATV, Martin Mwakiposa amesema kuwa mchezo kati ya Klabu ya Yanga na Namungo FC hautakuwa mwepesi kwa Wananchi kwani Wauaji wa Kusini wamekuwa wakiipa changamoto kubwa timu hiyo.

Mchezo huo wa raundi ya tatu ya Ligi Kuu ya NBC unatarajiwa kupigwa kesho Jumatano, Septemba 20, 2023 katika Dimba la Azam Complex, Chamazi.

"Ukifuatilia rekodi ya Yanga na Namungo ni miongoni mwa mechi ambazo zinakuwa ngumu sana si away wala nyumbani, ni mojawapo ya mechi ambazo Yanga huwa napata ugumu sana.

"Na ukitazama Namungo kwa jinsi walivyoanza ligi msimu huu hawakuanza vizuri sana, kwahiyo kwa vyovyote vile wanahitaji matokeo kwahiyo nategemea kuona ni mchezo ambao utakuwa mgumu lakini mzuri," amesema Martin Mwakiposa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: