Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wana jambo lao Bungeni

JENGO LA BUNGE NA WATU Yanga wana jambo lao Bungeni

Fri, 18 Feb 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Klabu ya Yanga leo Feb 18 itafanya uzinduzi wa kadi mpya za Uanachama za kielektroniki kwa Wabunge wa Bunge Ia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Wanachama wa Yanga.

Uzinduzi wa kadi za Kielektroniki ni sehemu ya mchakato wa mabadiliko ya kidigitali na ya mfumo wa uendeshaji wa Klabu kwa mujibu wa katiba ya Yanga toleo Ia 2021.

Hafla ya uzinduzi huo itafanyika kwenye Hoteli ya Morena jijini Dodoma kuanzia saa 4:00 asubuhi ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson.

Hafla hiyo itahudhuriwa na Waheshimiwa Wabunge, Viongozi wa Klabu ya Yanga, wadau na waandishi wa habari.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz